Sambaza....

Imeripotiwa kwamba Klabu ya soka ya Manchester United imeendelea kufanya mazungumzo na beki wa kati ya klabu ya Fiorentina inayoshiriki ligi kuu nchini Italy (Seria A) Nikola Milenkovic hata Baada ya Jose Mourinho ambaye ndiye alikuwa akimuhitaji kuondoka klabuni hapo.

Beki huyo amekuwa akifuatiliwa na Skauti wa Manchester United kwa vipindi mbalimbali mwaka huu hadi kufikia hatua ya aliyekuwa kocha wao Jose Mourinho kuamua kuhudhuria mchezo wa Serbia dhidi ya Montenegro mwezi Oktoba Ili kujiridhisha kiwango chake.

Baaada ya mchezo huo Mourinho aliuomba Uongozi wa klabu kumjumuisha kwenye Usajili wa January na mpaka sasa inaaminika kuwa mkurugenzi mtendaji wa Manchester United Ed Woodward yupo kwenye mazungumzo na wawakilishi wa beki huyo raia wa Serbia.

Mpaka sasa kocha wa muda Ole Gunnar Solskjaer hatokuwa na mamlaka makubwa katika Usajili wa January huku maamuzi makubwa yakiachwa kwa mabosi wake, ambao bado wanamuona Milenkovic kama chaguo la awali katika kuimarisha safu yao ya ulinzi.

Milenkovic amecheza michezo 16 ya ligi msimu huu akiwa na Fiorentina na katika michuano ya kombe la Dunia iliyofanyika mwaka huu nchini Russia alikuwa ni mchezaji tegemeo wa Serbia.

Sambaza....