Sambaza....

Kamati ya uchaguzi ya TFF iliyopewa mamlaka ya kusimamia uchaguzi mkuu wa Yanga na BMT imetangaza rasmi kuwa uchaguzi mkuu wa Yanga utafanyika tarehe 12 mwezi wa kwanza mwakani.

Na fomu za kugombea uchaguzi huo zitaanza kuchukuliwa kuanzia kesho. BMT iliwata TFF wasimamie uchaguzi wa Yanga baada ya waziri wa Habari, Utamaduni na Michezo, Harrison Mwakyembe kufanya mazungumzo na pande zote zinapingana Yanga.

Katika mazunguko yake aligundua suluhisho kubwa ni kufanya uchaguzi kuziba nafasi ambazo ziliachwa wazi na viongozi waliojiudhuru.

Viongozi ambao wametangaza kuachia Ngazi katika klabu hiyo ni pamoja na mwenyekiti wa klabu hiyo, Yusuph Manji, mwenyekiti msaidizi, Clement Sanga, pamoja na wajumbe mbalimbali wa kamati tendaji.

Hivo BMT iliwataka TFF kwa mujibu wa katiba ya TFF na Yanga kusimamia uchaguzi huo na Leo wametangaza rasmi uchaguzi huo kufanyika tarehe 12 mwezi wa kwanza mwakani na fomu kuanza kuchukuliwa Leo.

Sambaza....