Ligi kuu Tanzania bara inaendelea , huku ushindani ukiwa mkubwa. Huwezi kuacha kutaja ushindani bila kuacha kuwaongelea Simba na Yanga. Hawa ndiyo wazazi wa mpira wetu. Mpaka sasa timu hizi zimeshaonesha uwezo wao, lakini kuna tofauti moja tu inayowatofautisha wawili hawa. Tofauti hiyo ni Upana wa vikosi viwili.
UPANDE WA GOLIKIPA.
Simba inajivunia kuwa na magolikipa wawili ambao wanauzoefu na uwezo mkubwa ambao ni Aishi Manula na Deo Munish “DIDA”. Hawa ni magolikipa wenye uzoefu, Deo Munish ” DIDA” ashawahi kuwa golikipa wa timu ya taifa na Aishi Manula kwa sasa ni golikipa wa timu ya taifa. Hii ni tofauti na kwa upande wa Yanga, ambao wana golikipa mmoja ambaye anaonekana kama Golikipa mwenye kuaminika pekee, Beno Kakolanya ambaye mara nyingi husumbuliwa na majeruhi. Magolikipa wa ziada wa Yanga hawana kiwango cha kukaliabiana na Beno kakolanya. Ramadhani Kabwili ni Golikipa kijana ambaye hana uzoefu sana na Kindoki ni golikipa mwenye makosa mengi binafsi.
MABEKI
Simba wana mabeki wengi wenye kiwango kikubwa ambacho kinafanana sana tofauti na mabeki wa Yanga ambao viwango vyao vinapishana kwa kiasi kikubwa. Mfano, Kiwango cha Gadiel Michael ni cha kiwango cha juu ukilinganisha na cha Haji Mwinyi ambaye anacheza upande wa kushoto, ilihali Simba mabeki wa kushoto wanakiwango ambacho hakijapishana sana (Asante Kwasi na Mohammed Hussein).
Hata kwa upande wa mabeki wa kati, Simba inautajiri mkubwa wa mabeki ambao wanakiwango kikubwa tena kinachokaribiana tofauti na kwa upande wa Yanga.
VIUNGO
Hapa ndipo ubora wa Simba ulipo, Simba ina viungo bora na ina idadi kubwa ya viungo. Mfano, kabla ya mechi ya Jana dhidi ya Ruvu Shooting, mechi mbili zilizopita, Said Khamis Ndemla alicheza katika eneo la kiungo wa kuzuia, eneo ambalo hucheza Jonas Mkude. Na Said Ndemla alicheza vizuri sana na Simba haikutetereka.
USHAMBULIAJI.
Eneo hili Simba ina utajiri sana, na ina wachezaji ambao wana kiwango kikubwa. Yanga inaonekana inamtegemea sana Makambo eneo lile la mbele, tofauti na Simba ambayo ina utajiri wa kina Emmanuel Okwi, John Bocco, Adam Salamba,Meddie Kagere, ambao wote wanaviwango vikubwa kuliko washambuliaji wa akiba wa Yanga.