Sambaza....

Kocha wa zamani wa timu ya Taifa ya Italy Gian Piero Ventura ameteuliwa kuwa kocha mkuu wa timu ya soka ya Chievo Verona inayoshiriki ligi kuu ya nchini Italia ikiwa ni masaa machache baada ya Lorenzo D’Anna kufutwa kazi kutokana na matokea mabovu.

Ventura alikuwa hana kibarua toka mwezi Novemba mwaka jana alipofutwa kazi na shirikisho la soka nchini Italy kufuatia timu ya Taifa kushindwa kufuzu kwa mara ya kwanza baada ya miaka 60 kwenye michuano ya kombe la Dunia iliyomalizika miezi michache iliyopita nchini Russia.

Kocha huyo mkongwe mwenye umri wa miaka 70 amesaini mkataba wa miaka miwili na klabu hiyo yenye maskani yake kwenye mji wa Verona ambao kwa sasa wapo mkiani mwa msimamo wa Seria A, wakiwa na alama Hasi moja baada ya kukatwa alama tatu mwezi uliopita kutokana na kushindwa kuandika hesabu za klabu.

“Gian Piero Ventura ndiye kocha wetu mkuu, tunamtakia kila kheri katika kufanikisha majukumu yake,” Taarifa ya klabu hiyo imeeleza, ikimtangaza kocha huyo wa zamani wa vilabu kama Napoli, Sampdoria, Udinese na Hellas Verona, na mchezo wake wa kwanza utakuwa dhidi ya Atalanta Oktoba 21.

Sambaza....