Kuna ule usiku ambao ni ngumu kutoka kwenye kumbukumbu za mwanadamu, usiku ambao huacha alama. Ule usiku ambao mwanaume anaweza kupata nafasi ya kula chakula cha pamoja na mwanamke anayempenda.
Usiku ambao hubadilisha maisha ya mwanadamu kutoka katika daraja la umasikini na kwenda kwenye daraja la utajiri. Ni usiku ambao hutokea mara chache sana kwenye maisha ya mwanadamu.
Ndiyo usiku ambao ulitokea miaka minne iliyopita baada ya Loris Karius kuwapa zawadi nzuri Realmadrid kwenye fainali ya ligi ya mabingwa barani ulaya. Imepita tangu Realmadrid waifunge Liverpool, leo hii wanakutana tena kwenye usiku unaotengeneza kumbukumbu zisizofutika.
Usiku ambao umemfanya Carlo Ancellotti aweke kumbukumbu za kuwa kocha pekee kufika fainali 5 na inawezekana akawa kocha wa kwanza kuchukua makombe manne na kuwazidi Bob Paisley na Zinedine Zidane ambao kila mmoja wamechukua kombe hili mara tatu.
Ndiyo usiku ambao Karim Benzema, Luka Modrić, Dani Carvajal, Isco and Marcelo wanaweza kumfikia Cristiano Ronaldo kwenye rekodi yake ya kuchukua kombe la ligi ya mabingwa barani ulaya mara tano. Nausubiri usiku kuona kama Liverpool watazuia kumbukumbu hii kuwekwa.
Realmadrid ndiye timu pekee yenye mafanikio kwenye michuano hii ikiwa imechukua makombe 13 ikifuatiwa na AC Milan yenye makombe 7. Barcelona, Bayern Munich and Liverpool wote wakiwa wamechukua kombe hili mara 6.
Vilabu kutoka Hispania ndiyo vimechukua mara nyingi kombe hili, vikiwa vimechukua mara18 vikifuatiwa na vilabu kutoka England ambavyo vimechukua mara Behind 14 na vilabu kutoka Italy vikiwa vimechukua mara 12.
Juventus ndiyo klabu ambayo imefungwa mara nyingi kwenye fainali ya ligi ya mabingwa barani ikiwa imefungwa katika fainali 7.
Francisco Gento mchezaji wa zamani wa Realmadrid ndiye mchezaji ambaye ameshinda mara nyingi kombe hili akiwa ameshinda mara 6.
Cristiano Ronaldo ndiye mchezaji pekee aliyefunga magoli mengi kwenye michuano hii (140), akiwa n hat tricks nyingi kuzidi wachezaji wote (8),ndiye mchezaji ambaye amefunga magoli mengi ndani ya msimu mmoja (17 msimu wa 2013-2014), ndiye mchezaji ambaye ameweka kumbukumbu ya kufunga hattricks nyingi kwenye msimu mmoja(3 msimu wa 2015-2016) na ndiye mchezaji ambaye amefunga penalties nyingi kwenye michuano hii, akiwa amefunga penalties 15.
Inawezekana michuano hii ilizaliwa kwa ajili yake lakini kwa bahati mbaya usiku wa leo hatokuwepoe, ila itakuwepo timu ambayo huwa ina vina saba na michuano hii. Swali kubwa linabaki nani ataweka kumbukumbu nzuri usiku wa leo, kumbukumbu ambazo zitabaki na kusimuliwa kwenye vizazi vijavyo?