1. Jamaa aliikataa timu ya taifa ya Mali na kuamua kuichezea Ufaransa, huku viongozi wa shirikisho la soka nchini Mali wakijaribu mara mbili kumshawishi Kante kuchezea timu yao lakini aligoma, ingawa alizaliwa Ufaransa wazazi wake ni Raia wa Mali
2. Kwa sasa Kante ni mmoja ya wachezaji wanailipwa vizuri, akiwa anapokea kitita cha pauni 110,000 huo ukiwa ni mara mbili ya ule aliokuwa akipokea Leicester city
3. Sio mchezaji mwenye vituko vingi nje ya uwanja, hata marafiki zake wamekuwa wakimzungumzia kuwa ni mpole sana lakini ndani ya uwanja ni balaa lingine
4. Udogo wa umbo lake ukikaribia kumnyima nafasi Leicester city, pale kocha msaidizi wa wakati huo Steve Walsh alipompeleka klabuni hapo haikuonekana kama angesajiliwa huku kocha mkuu wa wakati huo Craudio Ranieri akitilia mashaka umbo la Kante na ushindani wa ligi kuu ya uingereza
5. Kutokana na sura yake kuwa ya kitoto, alipofika kwenye uwanja wa mazoezi wa Leicester city kwa mara ya kwanza viongozi wa klabu hiyo walimuuliza ” umekuja kumtafuta nani hapa?”
6. Kante alikataa ofa ya Jose Mourinho, wakati wa usajili wa majira ya kiangazi Manchester United ilikuwa miongoni mwa klabu zilizohitaji huduma ya mchezaji huyo, lakini Kante aliamua kwenda darajani
7. Wakati Dunia nzima ikimtambua Kante kocha wa Chelsea Antonio Conte, alisema kuwa jina hilo lilikuwa geni kwake kabla ya kukutana Stamford Bridge
8. Bao lake la kwanza kufunga akiwa timu ya taifa ya Ufaransa, ilikuwa ni kwenye mchezo dhidi ya Russia ambapo aliiwezesha kuibuka na ushindi wa mabao 4-2 kunako dimba la Stade De France
9. Katika msimu wa kwanza akicheza kwenye ligi 1 hakuna mchezaji aliyepokonya mipira mara nyingi zaidi ya Kante
10. Kante ni shabiki mkubwa wa msanii wa kike nchini Marekani mwanadada Rihanna